chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys,
imeondoka Dar es Salaam mchana wa leo kwa
Ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda
Morocco kupitia Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Timu hiyo yenye wachezaji 23 na viongozi wanane
imepanda ndege muda mchache uliopita katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dar es Saalam.
Kabla ya kusafiri, timu hiyo ilikuwa kambini hapa
nyumbani tangu Januari 29, mwaka huu na baada
ya kambi ya mwezi mmoja na nusu, ilicheza mechi
tatu za kirafiki za kimataifa.
Machi 30, 2017 ilicheza Burundi ‘Intamba
Murugamba’ na kushinda mabao 3-0 kabla ya
kurudiana tena Aprili 1, mwaka huu na kushinda
mabao 2-0. Mechi zote mbili zilifanyika Uwanja wa
Kaitaba, ulioko Bukoba mkoani Kagera.
Mechi ya mwisho hapa nyumbani ilifanyika Aprili 3,
mwaka huu dhidi Ghana ‘Black Starlets’ na kutoka
sare ya 2-2 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Serengeti Boys ilitumia mchezo huo kama ishara
ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya
kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia
Mei 14, mwaka huu.
Serengeti Boys itakuwa Rabat, Morocco kufanya
kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5,
mwaka huu. Ikiwa huko angalau itacheza mechi za
kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji
morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au
Misri.
Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi,
mwaka hu ambako timu itasafiri hadi Cameroon.
Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za
kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na
6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu
kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa
kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.
Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo
baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye
kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys
kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri
kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki
zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon
na Guinea.
Kila la kheri Serengeti Boys katika mapambano ya
kuwania ubingwa wa Afrika kadhalika kucheza
fainali za Kombe la Dunia hapo Novemba, mwaka
huu zitakazofanyika India. Serengeti Boys inaweza
na Mtanzania tunakuomba kuichangia timu hii kwa
namna ya 223344 kupitia mitandao yote ya simu.
Chapisha Maoni