0
BAO pekee la kiungo
Mzimbabwe, Thabani Scara
Kamusoko limeipa Yanga
ushindi wa 1-0 katika
mchezo wa kwanza wa
mchujo wa kuwania kuingia
hatua ya makundi ya Kombe
la Shirikisho Afrika jioni ya
leo Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Rasta huyo alifunga bao hilo
dakika ya 61 akimalizia pasi
ya kiungo mshambuliaji
Mzambia, Obrey Chirwa
baada ya kazi nzuri ya
kiungo Mnyarwanda Haruna
Niyonzima aliyepasua na
mpira kutokea nyuma.
Yanga sasa itahitaji sare
katika mchezo wa marudiano
wiki ijayo mjini Algiers.
Algeria ili kwenda hatua ya
makundi ya kombe la
Shirikisho kwa mara ya pili
mfululizo mwaka huu.
Katika mchezo huo
uliochezeshwa na marefa
kutoka Rwanda, Louis
Hakizimana aliyeyepuliza
filimbi akisaidiwa na washika
vibendera Theogene
Ndagijimana na Jean Bosco
Niyitegeka, Yanga ilipoteza
nafasi nzuri zaidi ya tatu za
kufunga kipindi cha kwanza.
Africa Newss Sports

Baada ya mchezo kuanza
taratibu kwa timu zote
kusomana, MC Alger
walikuwa wa kwanza
kulijaribu lango la Yanga
baada ya shuti la Goveri
Kaled kudakwa na kipa
Chaouch Faruzi.
Yanga waliotumia mfumo wa
4-3-3 wakishambulia na
Deus Kaseke, Simon Msuva
na Obrey Chirwa wakalitia
majaribu kwa mara ya
kwanza lango la MC Alger
dakika ya 15, lakini kiungo
Haruna Niyonzima
akachelewa kuiwahi krosi ya
beki Hassan Kessy.
Baadaye Yanga wakabadilika
na Kaseke akarudi kucheza
kama kiungo huku Kamusoko
akisogea katikati kucheza
kama mshambuliaji pacha wa
Chirwa na hapo ndipo
mabingwa hao wa Tanzania
walipoanza kuwaamsha
mashabiki wao kwa kosa
kosa za kusisimua.
Winga Simon Msuva alitia
krosi nzuri dakika ya 29,
lakini mshambuliaji Obrey
Chirwa akapiga fyongo mpira
ukapotelea kwenye himaya
ya wapinzani na kuondoshwa
kwenye hatari.
Msuva tena akatia krosi
dakika ya 28 na pamoja na
kumfikia kiungo Mzimbabwe,
Thabani Kamusoko akapiga
nje akiwa kwenye boksi.
Chirwa naye akapata pasi
nzuri ya Mwinyi Hajji
Mngwali upande wa kushoto
wa Uwanja dakika ya 44,
akaingia ndani vizuri na
kupiga shuti zuri, lakini
likaende nje upande wa pili
wa lango sentimina chache
tu.
Kamusoko tena akaikosesha
Yanga bao dakika ya 45 na
ushei baada ya kupiga juu ya
lango kufuatia pasi nzuri ya
Msuva.
Kipindi cha pili, kocha
Mzambia wa Yanga alianza
na mabadiliko akimpumzisha
kiungo Deus Kaseke na
kumuingiza mshambuliaji
Mzimbabwe Donald Dombo
Ngoma aliyekwenda
kuongeza kasi ya
mashambulizi ya wan
Jangwani.
Kikosi cha Yanga SC
kilikuwa; Deogratius Munish
‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi
Mngwali, Vincent Bossou,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Said Juma ‘Makapu’, Simon
Msuva, Thabani Kamusoko,
Obrey Chirwa, Haruna
Niyonzima/Emanuel Martin
dk82 na Deus Kaseke/
Donald Ngoma dk56.
Mo Alger; Chaouch Faruzi,
Hachoud Abdullman, Karaovi
Amir, Mebarakou Zidane,
Bouhenna Richid, Kacem
Mehdi, Chrifei Hichem,
Bougueche Hajj/Feedbad
Zahir dk85, Derarya Warid/
Awady Said dk76, Goveri
Kaled/BemmouAbdulcheri
dk74 na Nekkache Hichem.

Chapisha Maoni

 
Top