
Hatua hiyo ilithibitishwa siku ya Jumanne mjini Bahrain. Kwa sasa bara hilo lina nafasi 5 pekee.
Taifa la kumi la Afrika litashiriki katika mchuano wa muondoano utakaojumuisha mataifa sita ili
kuamua kuhusu nafasi mbili.
Baraza la Fifa lilipendekeza vile litakavyotoa nafasi hizo 48 mnamo tarehe 30 mwezi Machi. Kinyang'anyiro hicho kipya kitashirikisha timu 16
kutoka Ulaya.
Wanachama wa Fifa walipiga kura mnamo mwezi Januari kuongeza timu zitakazoshiriki kutoka 32 hadi 48 kuanzia dimba la mwaka 2026.
Chapisha Maoni