Ndikumana amefurahia hatua ya timu
hiyo kutinga Nusu Fainali ya
Michuano ya Kombe La Shirikisho
(Azam Sports Federation Cup) na
kusema kuwa wako tayari kukabiliana
na Simba katika fainali Baadaye mwezi
huu.
Ndikumana amesema ushindi huo
Umeonyesha uwezo mkubwa Mbao Fc
wanao wa kuendelea kufanya vizuri
katika michuano mbali mbali ndani na
nje ya nchi. Mbao tuna uwezo
-Tumefurahi sana kwa sababu
tumeweza kuonyesha uwezo wetu na
kuwa Mbao si timu
ndogo,tumeonyesha uwezo wetu licha
ya kwamba wengi wetu ni chipukizi
tumeonyesha kuwa Timu ndogo
inaweza kuwa na uwezo mkubwa
kama timu zingine,amesema
Ndikumana.
Kuhusu fainali dhidi ya Simba
Ndikumana amesema ni Mechi
ambayo Mbao wanaitarajia kwa hamu
na gamu Ili kumaliza kisasi dhidi ya
timu hizo mbili. Kulipiza kisasi
-Ni mechi nzuri tunaisubiri ni kama
ya kulipiza kisasi dhidi ya Simba
lakini si kisasi tunataka tumalize kazi
tuliyoianza ya kumaliza Simba,
ameongeza Nahodha huyo raia wa
Burundi.
Mbao walifuzu kwa Fainali ya FA kwa
mara ya kwanza kwa kuwatupa nje
Mabingwa watetezi wa taji hilo Yanga
SC kwa kuwashinda kwa 1-0 katika
mchezo ambao ulifanyika Jumapili
kwenye uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
Chapisha Maoni