Haroub 'Cannavaro '.amewaahidi
Ubingwa wa Ligi Kuu mashabiki wa
klabu hiyo na kuwaomba wasipoteze
matumaini na timu hiyo licha ya
kutolewa na Mbao kwenye fainali ya
Kombe La Shirikisho (Azam Sports
Federation Cup ),na kuwaahidi kuwa
Yanga itashinda ubingwa wa Ligi Kuu
Soka Tanzania Bara.
Cannavaro amekiri kuumizwa na
matokeo hayo ambapo walipoteza
mchezo huo kwa Mbao na kusema
Kuwa walikuwa wamejipanga vizuri na
walitarajia ushindi. Mashabiki kuwa na
subira
Hatukutarajia kupoteza
-Tulikuwa tumejiandaa vizuri
tulicheza vizuri na tulipata nafasi
nyingi za wazi lakini hatukufanikiwa
kufika hatua ya Fainali, huu ni mpira
na wakati mwingine tunapata matokeo
ambayo hatukutarajia, amesema
Cannavaro.
Aidha amewaomba Mashabiki wao
kuendelea kuwaunga mkono na
kuwaahidi kuwa watatetea ubingwa wa
Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Kutetea ubingwa wa Ligi Kuu
-Bado tuna nafasi ya kuwafurahisha
mashabiki wetu tutaelekeza nguvu
zetu kwa michezo ya Ligi iliobaki
tutajitahidi tutafanya vizuri na kutetea
ubingwa wetu ,ndoto yetu ya
kushiriki kwenye Michuano ya Klabu
Bingwa bado ipo ndio maana
nawaomba mashabiki wetu wasife
moyo, ameongeza nahodha huyo.
Yanga ambao ni Mabingwa watetezi
wa Ligi kuu watahitaji kushinda Ligi Ili
kupata nafasi ya kuwakilisha kimataifa
msimu ujao baada ya Kuondolewa na
Mbao kwenye fainali ya Kombe La
Shirikisho ambapo Mshindi wa
michuano hiyo pamoja na kushinda
shilingi milioni 50 anapata fursa
kuwakilisha katika michuano ya
Kombe La Shirikisho Barani.
Nafasi ya pili
Yanga ambao wako katika nafasi ya
pili wakiwa na alama 56 wamebakiwa
na michezo minne dhidi ya Toto
Africans, Mbeya City, Tanzania Prisons
na Mbao Fc.
Chapisha Maoni