0

Bilionea Mohammed Dewji ametimiza ahadi yake
kwa klabu ya Simba baada ya kutoa Sh milioni
100 kusaidia usajili.
Mo ametoa fedha hizo leo na kuzikabidhi kwa Rais
wa Simba, Evans Aveva.
Mo alikubali kuisaidia Simba katika usajili wakati
mchakato wa kwenda kwenye mabadiliko na kuwa
kampuni ukiendelea.
Tayari bilionea huyo kijana ametangaza kumwaga
fedha Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51 ya
umiliki wa klabu hiyo na wanachama wameridhia
katika mkutano wa wanachama uliofanyika juzi
Jumapili.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top