0

Chipukizi kiungo cha kati wa Ujerumani Leroy Sane
amekamilisha uhamisho kwenda Manchester City
kwa gharama ya pauni milioni £37m.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 ametia
sahihi kandarasi ya miaka 5 baada ya kutokea
Schalke O4.
Meneja mpya wa Man City Pep Guardiola
amemmiminia sifa kedekede kiungo huyo akisema
kuwa ana kasi na kipaji cha kipekee.
'' ninaamini kuwa jinsi anavyocheza huyo kijana
inaonesha wazi kuwa anatalanta ya kuvutia sana ,
ninatarajia mashabiki wetu watavutiwa na hulka
yake''
Sane, aliisaidia Ujerumani kutinga nusu fainali ya
mchuano wa Euro 2016, aliifunga klabu yake ya
Schalke mabao 33 katika ligi kuu ya Ujerumani.
Schalke ilimaliza msimu katika nafasi ya 5.
''ukimtizama akicheza unavutia na ueledi wake ,
yaani hababaishwi na mpira wala hasuisui hata
anapopewa mpira katika mazingira magumu''
alisema Guardiola.
''Hivi unavyomuona ana umri wa miaka 20 tu lakini
tayari ameshajishindia nafasi katika timu ya taifa
,hiyo inatudhihirishia kuwa anakipaji kinachohitaji
kunolewa kisha anawiri kitaaluma''
Kwa upande wake Sane amesema kuwa moja ya
sababu kuu yake ya kujiunga na Man City ni
kupata nafasi ya kujifua chini ya ukufunzi wake
Guardiola.
" Wakati huu katika taaluma yangu hii bila shaka
Guardiola ndiye kocha ambaye ninahakika atanifaa
zaidi na kunikuza'' alisema Sane.
''Sitarajii kupewa nafasi moja kwa moja ila najua
baada ya muda nitapata nafasi''



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top