0

Jembe jipya la Azam FC limeshatua Chamazi na
kukabidhiwa jezi nambari 10 iliyokuwa kivaliwa
na Kipre Tchetche, mambo yameiva sasa
Kocha Mkuu wa Azam FC Zeben Harnandez
amemtambulisha rasmi mshambuliaji mpya wa
timu hiyo Mghana Enoch Atta Agyei aliyesajilowa
hivi karibuni kutoka Medeama.
Hernandez amemkabidhi mchezaji huyo jezi
namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Kipre
Tchetche aliyetoweka kwenye timu hiyo pasipo
taarifa za msingi.
"Ameanza leo mazoezi na wenzake na
ameonyesha kufanya vizuri ni imani yangu
atafanya vizuri kutokana na utayari aliokuwa nao
ukizingatia alikuwa akishiriki mashindano
makubwa," amesema Hernandez.
Kukabidhiwa jezi namba 10 ni wazi Azam itakuwa
imeachana na Tchetche anayetajwa kujiunga na
Yanga.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top