0
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu baada ya leo kuwafunga wenyeji, Cameroon 1-0 mjini Yaounde.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ahmadou Ahijo, mjini Yaounde na kuhudhuriwa na gwiji wa soka wa Cameroon, Rogger Milla, bao
la Serengeti Boys limefungwa na Ally Ng'anzi dakika ya 36.
Serengeti Boys ilitua Younde, Cameroon Alhamisi ikitokea mjini Rabat, Morocco ambako iliweka kambi ya karibu mwezi mmoja na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon na kushinda 2-1
kila mchezo.

Chapisha Maoni

 
Top