Michezo mitano katika ligi kuu ya soka nchini England imechezwa leo huku matokeo tofauti yakipatikana.
Mchezo wa mwanzo kabisa leo ulizikutanisha Manchester United na Swansea City na mpaka mchezo unamalizika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 Magoli ya Wayne Rooney kwa United na Gyfil Sidgusson kwa Swansea.
Chelsea wakiwa ugenini walionyesha nia yao ya kuchukua ubingwa msimu huu wakiifunga timu ngumu ya Everton bao 3-0 magoli ya Pedro,Gary
Cahill na Willian. Middlesbrough ikicheza Nyumbani iliweza kuibania
Manchester City na kutoka sare ya bao 2-2 Mchezo muhimu kwa Man City kuweza kusonga mbele katika nafasi 3 za mwanzo.
Mchezo wa mwisho leo ulikua ni London Derby baina ya wenyeji Tottenham Hotspurs na Arsenal
mchezo uliomalizika kwa Arsenal kufungwa bao 2-0.
Magoli ya Delle Alli na Harry Kane aliyefunga kwa penati yalitosha kuwapa Tottenham mwanga wa
kulitafuta kombe msimu huu wakizidiwa na Chelsea kwa pointi 4 mpaka sasa kwenye msimamo.
Chapisha Maoni