mwaigizaji wa filamu na mtafutaji
kunako tasnia ya muziki wa Bongo
Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’,
kuvalishwa pete ya uchumba na
mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu
Mziwanda’ tayari watu wameanza
kuisengenya.
Shilole alivalishwa pete hiyo katika
sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika
katika ‘apartment’ za Baraka Plaza,
Mikocheni jijini Dar ambapo mara
baada ya mwanadada huyo kukata
keki na kuwalisha watu mbalimbali
waliohudhuria, ndipo Nuhu
alipomsapraizi mwanadada Shilole
kwa kumvisha pete hiyo.
Kitendo hicho kilionekana kukubalika
na waalikwa wengi, lakini wengine
hawakufurahishwa nacho kwa madai
eti kwamba Nuhu ni mdogo kuliko
Shilole hivyo hakustahili kuvisha pete
mtu mwenye umri kama dada’ke.
“Mh! Mwenzangu hii kali, mimi siku
zote Nuhu niliamini hayupo serious
kutembea na Shilole maana ni
mkubwa kuliko yeye lakini sasa hapa
kanishangaza kweli, kwa nini asitafute
mdogo mwenzake?,” alisikika dada
mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja
jina lake.
Hata hivyo licha ya masengenyo hayo
kusambaa chini kwa chini, Nuhu
aliwakata watu vilimilimi kwa
kutamka hadharani kuwa
wanapendana na Shilole hivyo haoni
ajabu kama kuna watu
hawatakubaliana na penzi lao.
“Tukio linalotendeka hapa limepewa
baraka zote na wazazi wetu
wameridhia mimi na mchumba wangu
tuoane na hii ni hatua ya kwanza tu
mengine yatafuata na msishangae
sana kuona wazazi wetu hawapo eneo
hili ni kwamba wanatambua
kinachoendelea hapa.
“Najua wengi mtakuwa na maswali
kuhusu hili, mimi na yeye
tunapendana na ndiyo maana leo hii
namvisha pete mpenzi wangu na
Mungu atatujaalia katika maisha
yetu,” alisema Nuhu na sherehe
ikaendelea kwa watu kula na kunywa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa
mbalimbali akiwemo Steven Mengere
‘Steve Nyerere’, Wellu Sengo
‘Matilda’, Shettah, Martin Kadinda,
Mh. Temba, Chegge, DJ Choka na DJ
Tass.
Steve Nyerere aliyekuwa MC wa
shughuli hiyo alisema Shilole ni
shemeji yake kwani yeye ni kaka yake
Nuhu, na kwamba tukio linalofanyika
hapo, wao kama ndugu
wamekubaliana na ndoa itafungwa.
“Siku zote huwa namwambia shemeji
yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa
hatua aliyofikia mpaka sasa na
ninamkubalisana shemeji yangu,
karibu Iringa,” alisema muongoza
sherehe huyo.
Chapisha Maoni