0
MWANAMKE mmoja wa Kitanzania
aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika
miji mbalimbali ya Tanzania, likiwemo
Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam na mingine ya Namibia, ameibuka na
kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya
kusambaza Ukimwi kwa wanaume
wakware.

Licha ya kukiri kufanya hivyo, akisema
kwa siku alipanga hadi wanaume
watano,tena bila ya kutumia kinga
akisema alidhamiria kuusambaza
ugonjwa huo hatari alioambukizwa
akiwa katika shughuli za ukahaba.
Alijigundua ameathirika mwaka 2006.

Hata hivyo, katika maelezo yake
ameelezea kuijutia dhamira yake hiyo,
akisema alisambaza kutokana na hasira
aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume
aliyemwambukiza.

“Nilimchukia sana kila mwanamume,
yeyote aliyejiita mwanamume…
nilishindwa tu kuwawinda na kuwaua,
lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia
silaha yoyote kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua…

“Ndani mwangu nilijisemea kamwe
sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote
anayekuja kwangu nammaliza. Kwa
namna walivyoniambukiza lazima
niwaambukize’.

"Sijui nimewaambukiza wanaume
wangapi, lakini ni maelfu,” alisema
mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana
umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda
wake kanisani nchini Nigeria hivi
karibuni.

Chapisha Maoni

 
Top