0

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ametunukiwa tuzo ya kocha bora Bodi ya Ligi Kuu England.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa Italia na Juventus, amepata tuzo hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa baada ya kukiongoza kikosi cha Chelsea kutwaa
ubingwa msimu wa 2016/17.
Ubingwa wa Chelsea ulianza kunukia tangu Machi baada ya kuanza kuchanja mbuga, huku wakiziacha timu zilizokuwa
zinaifuatia kwa pointi nyingi.
Chelsea imemaliza mashindano hayo ikiwa imekusanya pointi 93 na kushinda michezo 30 kati ya 38 ilyocheza msimu huu.
Hata hivyo, Conte ana nafasi ya kutwaa taji jingine la ndani kutokana na kuwa na mechi ya fainali ya Kombe la FA Jumapili wiki hii.
Chelsea watakuna na Arsenal kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali kwenye dimba la Wembley.


Chapisha Maoni

 
Top