0
Hali ya Nahodha wa Timu ya Simba
SC na Kiungo wa Timu ya Taifa ya
Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Jonas
Mkude aliyepata Ajali imethibitishwa
kuwa inaendelea Vizuri na muda
wowote anaweza kuruhusiwa kutoka
Hospitalini.
Meneja wa Taifa Stars Danny Msangi
amesema baada ya kupata Ajali hiyo
Jana walijitahidi Kutafuta
Kumuhudumia Jonas na walimfikisha
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambapo alipatiwa huduma nzuri na
mpaka sasa anaendelea vizuri.
-Tulikuwa wote na tulimfikisha pale
hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo
cha MOI mpaka hivi sasa Asubuhi Hii
naambiwa anaendelea Vizuri, japo
bado amelazwa" Alisema.
Vipimo.
- Madaktari Jana usiku walimfanyia
Kipimo cha City scan kuangalia labda
maumivu yoyote Ya ndani hasa
kichwani, Lakini ile picha ilionesha
hana maumivu makubwa, isipokuwa ni
msukosuko tu na michubuko Kidogo,
na wakashauri awekwe kwenye
ungalizi" Aliongeza Msangi.
Aidha Msangi Anasema kwamba
Mkude amemuambia kuwa Kwa sasa
anaendelea vizuri Tofauti na Hali
ilivyokuwa wakati wa Ajali na Kama
ataruhusiwa Mapema Basi atajiunga
na timu ya Taifa Mapema.
Ajali.
Ikumbukwe kwamba Mkude alikuwapo
kwenye Ajali ya watu Sita iliyotokea
Jana katika eneo la Dumila, nje
Kidogo ya Mji wa Morogoro ambapo
katika Ajali hiyo Mtu mmoja alipoteza
maisha Huku wengine watano
wakipata Majeraha madogodogo.
Mkude alikuwa akiwahi kambi ya Taifa
Stars ambapo walitakiwa kuondoka na
wenzao kuelekea nchini Misri
kujiandaa na Mchezo wa Kufuzu kwa
fainali ya Mataifa Afrika dhidi ya
Lesotho Mwezi ujao.

Chapisha Maoni

 
Top