0
Kikosi cha Timu ya soka ya Singida
United iliyopanda ligi kuu msimu huu
kimeanza mazoezi makali uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam kwa
maandalizi ya michuano ya SportPesa
Super itakayorindima nchini kuanzia
Juni 5.
Singida ambao wanajipanga vyema
kwa msimu mpya wa ligi kuu Soka
Tanzania Bara 2017/18 ikiwa ni mara
yao ya kwanza tayari wameanza
mazoezi katika uwanja wa Uhuru Jijini
Dar na wakitamba kuitumia michuano
hiyo kujitathimini uwezo wao baada ya
kufanya usajili mzuri ndani na nje ya
nchi.
Tayari wachezaji wao toka nje ya nchi
wamewasili nchini kwa ajili ya
michuano hiyo ambayo wao wanaipa
Umuhimu mkubwa wa kujenga umoja
kitimu na masuala mengine ya
kiufundi.
Mwalimu mkuu wa timu hiyo bwana
Hans Van Pluijm ambaye aliwika
vyema na mabingwa wa ligi kuu
Tanzania bara, Dar Young Africans
amesema ataitumia michuano hiyo
kuwatizama vijana wake ambao kwa
asilimia 80 ni kikosi kipya na baada
ya hapo wataingia kwenye kambi
maalumu ndani au nje ya nchi kwa
ajili ya kukisuka kikosi chake kiwe cha
ushindani Kwenye ligi kuu.
Wazingatie Kanuni tu.
-Mara nyingi timu ambazo zinapanda
ligi kuu kwa mara ya kwanza, msimu
wao wa kwanza hulenga kubakia ligi
kuu na sio kutwaa ubingwa lakini
nawaandaa vijana wangu kutwaa
ubingwa wa ligi kuu na kombe la
ASFC, Naijua vyema ligi ya hapa
kikubwa wasimamizi wa ligi
wazingatie kanuni na sheria kwa
vilabu vyote" alieleza kocha huyo.
Kampuni ya Bahati Nasibu ya
SportPesa toka nchini Kenya
Imeandaa michuano ambayo
itashirikisha jumla ya Timu nane
ambazo ni Tusker FC, AFC Leopards,
Nakuru all Stars na Gor Mahia zote
toka Kenya, Pamoja na wakongwe wa
soka nchini Yanga SC, Simba SC na
wageni hawa wa ligi kuu Singida
United, pamoja na Jang'ombe Boys,
Ambapo Bingwa atajipatia kiasi cha
shilingi Milioni 60.

Chapisha Maoni

 
Top