0
Shirikisho la Soka Nchini Tanzania
(TFF),imesema kuwa haijapokea barua
yeyote kutoka FiFA kuhusu rufaa
iliyowasilishwa na Klabu ya Simba na
kuwa barua ambayo imekuwa
ikisambaa mitandaoni kuhusu majibu
ya rufaa hiyo si ya kweli.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas
amesema kuwa TFF haijapokea barua
ya majibu ya rufaa ya klabu ya Simba
kutoka FIFA na kuwa wanasubiri na
kama watapokea barua hiyo watatoa
taarifa rasmi.
Hatujapokea barua
Aidha kumekuwa na barua ambayo
imekuwa ikisambaa mitandaoni ikiwa
na anwani ya FIFA, barua hiyo
ilionekana kuwa majibu ya Simba
kutoka FIFA ambapo ilionekana
kuridhishwa na maamuzi ya awali ya
TFF ya kuwarudishia Kagera Sugar
pointi zake tatu ambazo walikuwa
wamepokwa na kamati ya Masaa 72
kwa madai walimchezesha mchezaji
Mohamed Fakhi ambaye alikuwa na
kadi tatu za njano kinyume na sheria
na Kanuni za ligi hiyo kwa kusema
hakuna haja ya kufanya mabadiliko
katika maamuzi hayo.
Kutoridhishwa
 Rufaa Klabu ya Simba iliwasilisha
kesi yake kwa FIFA baada ya
kutoridhishwa na maamuzi ya kamati
ya Katiba Sheria na Hadhi ya
Wachezaji ambao walisema Simba
haikukidhi vigezo walipowasilisha kesi
hiyo dhidi ya Kagera Sugar.

Chapisha Maoni

 
Top