Mganda Jackson Mayanja Mchezo wa
Mkondo wa Kwanza waliofungwa Bao
1-0 na African Lyon walicheza Vizuri
zaidi kuliko mchezo wa Jumapili
ambao wameibuka na ushindi wa
Mabao 2-1.
Mayanja amesema timu yake
haikucheza Vizuri na wamepata
mabao yote mawili kwa Makosa ya
African Lyon lakini mchezo huo
haukuwa mzuri ukifananisha na
mchezo uliopita Jambo ambalo
watalifanyia kazi katika Michezo miwili
iliyosalia.
-Mechi ya Kwanza tulikosa mabao
mengi zaidi kuliko mechi hii, na kama
mtakumbuka mwisho wa siku
walitufunga, hii mechi hatukucheza
vizuri inaonekana kabisa African Lyon
walikuwa makini zaidi katika Mchezo
huu kuliko ule wa Mwanzo,
tumeshinda kibahati’ Alisema
Mayanja.
Bao la Kujifunga.
Amesema isingekuwa bao la Kujifunga
la Hamad Juma la dakika ya 54 basi
mechi hiyo ingemalizika kwa sare
kwani African Lyon walikuwa makini
na wao Simba hawakuonesha kabisa
nia ya Kuibuka na Ushindi kutokana
na Mchezo wao.
-Tumekosa nafasi Mwanzoni lakini
tulipoa baadae , African Lyon ya Mara
hii ilikuwa Makini sana, Labda
kujifunga tu ndio imetupa ushindi,
lakini wao walikuwa makini zaidi yetu,
kama unavyojua mchezo wa Mpira ni
wa makosa Walifanya makosa na
Tumewaadhibu’ Aliongeza Mayanja.
Ushindi huo umewapa nafasi Simba
ya Kuendelea kupambana na Yanga
katika harakati za kuwania Ubingwa
wa Ligi kuu Msimu huu, kwani sasa
wamebakiwa na Michezo miwili na
wapo kileleni wakiwa na alama 62
huku Yanga waliobakiwa na michezo
mine wapo nafasi ya pili na alama 59.
Chapisha Maoni