0
Mbwana Samatta aliifungia timu yake ya Genk goli moja na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya AS Eupen
Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amefungaba bo la pili, timu yake, KRC Genk ikishinda 2-1 dhidi ya KAS Eupen Uwanja wa Luminus Arena, Genk kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi
ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
Samatta alianza katika mchezo huo na baada ya beki Mfinland, Jere Uronen kufunga bao la kwanza dakika ya 18, naye akafuatia kwa kufunga la pili dakika ya 28 akimaliza ukame wa mechi
tano za kucheza bila kufunga.
Eupen walipata goli lao pekee dakika ya 76 kupitia kwa H.C. Onyekuru na kupelekea mchezo kumalizika kwa Genk kuibuka washindi wa mchezo kwa magoli 2-1.
Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League mwakani kwa kufikisha pointi 19
baada ya kucheza mechi saba na Samatta jana ameichezea Genk mechi ya 56 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya
DRC akiwa amefunga mabao 19 sasa.

Chapisha Maoni

 
Top