0

TIMU ya Kagera Sugar leo
inatarajiwa kuwasilisha
malalamiko Bodi ya Ligi ya
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kupinga kadi nyekundu
aliyoonyeshwa mshambuliaji
wao, Mbaraka Yussuf Abeid
katika mchezo dhidi ya
Yanga jana.
Kagera Sugar ilifungwa 2-1
na wenyeji, Yanga SC katika
mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara jana
Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na bahati mbaya
mfungaji wa bao lao na
mshambuliaji wao tegemeo,
Mbaraka Yussuf hakumaliza
mechi.
Refa bora wa Ligi Kuu msimu
uliopita, Ngole Mwangole wa
Mbeya alimtoa nje kwa kadi
nyekundu Mbaraka Yussuf
Abeid dakika ya 87 baada ya
kumchezea rafu beki wa
Yanga, Kevin Yondan.


Mratibu wa Kagera Sugar,
Mohammed Hussein alisema
kwamba wanaandikia barua
TFF kupinga kadi hiyo kama
ilivyo walivyowahi kufanya
Yanga, kupinga kadi ya
Obrey Chirwa.
Alisema mchezaji wao
hakucheza rafu zaidi ya
kuruka juu tu kiungwana
kuwania mpira dhidi ya beki
wa Yanga, Yondan. “Yondan
pale alimdanganya refa, na
refa akadanganyika, lakini
naamini wakirudia kuangalia
teknolojia ya picha za video
wataona vizuri na
watabatilisha maamuzi
yao,”alisema.
Alisema kadi hiyo
itamkwamisha Mbaraka
katika harakati zake za
kuwania ufungaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara hadi sasa
akiwa ana mabao 12, nyuma
ya Simon Msuva wa Yanga,
anayeongoza kwa mabao
yake 13.


Chapisha Maoni

 
Top