0
Benchi la Ufundi la Timu ya Soka ya
Yanga ya Jijini Dar es Salaam
limesema limekoshwa na Kiwango
kilichoneshwa na wachezaji wao
katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar
na kuibuka na Ushindi wa Mabao
2-1.
Akizungumza na mtandao huu Kocha
msaidizi Juma Mwambusi Amesema
Kama Benchi la Ufundi limefurahishwa
na Kiwango hicho na kuwaomba
wachezaji wote wajitume zaidi katika
michezo iliyosalia ili watetee Ubingwa
wao.
-Wachezaji hakika wamecheza vizuri,
Licha ya Makosa madogo ya kipindi
cha kwanza na kuruhusu bao Lakini
dakika zote walikuwa makini, Kagera
Sugar walijitahidi Sana kupitia katikati
tuliliona na tukawaelekeza wachezaji
na wakafanya tuliyoaagiza" Mwambusi
Alisema.
Tumekosa Mabao Mengi.
Hata hivyo Mwambusi Amesema
wachezaji wake walikosa umakini
katika eneo la ushambuliaji Kwani
kama wangekuwa makini Basi
wangeondoka na Idadi kubwa ya
mabao.
-Tumekosa Mabao Mengi Ya wazi
wachezaji walikosa umakini na hilo
lazima tulirekebishe kwenye mchezo
ujao, Tunataka kutangazwa Mabingwa
Mapema, hivyo Inabidi tupunguze
Makosa" Alisema.
Yanga wapo Kileleni mwa Msimamo
wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara
wakiwa na alama 62 Sawa na watani
zao Simba Ila wakiwazidi kwa Tofauti
ya Mabao ya Kufunga na kufungwa,
hata hivyo Yanga wanamchezo mmoja
mkononi.

Chapisha Maoni

 
Top