0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dak Harrison Mwakyembe
amesema kuwa wizara hiyo itaweka
mikakati ya kuhakikisha kuwa
wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana
chini ya Umri wa Miaka 17 'Serengeti
Boys',vipaji vyao vinaendelezwa na
kutumika ipasavyo. Mwakyembe
ambaye aliyasema hayo wakati
akipokea mchango wa shilingi milioni
50 kutoka kwa kampuni ya Ubashiri
ya Sportspesa ambayo imeanza rasmi
Shughuli zake nchini Tanzania.
Tutawaendeleza
 -Hatutafanya makosa ambayo
yalifanyika huko nyuma ili kuweza
kuwalinda wachezaji wetu, hakuna
kijana atakayepotea hawa ni Mali ya
Taifa tunataka tuwapeleke Timu nzuri
ili kuona vipaji hizo zinaendelezwa
haitakuwa kama ilivyotokea huko
nyuma kulikuwa na timu nzuri za
vijana ambao zwalifanya vizuri lakini
hawajulikani walipo kwa
sasa,amesema Mwakyembe.
Aidha Waziri huyo amewaomba
wadau ,mashabiki na wapenzi wa timu
hiyo kuendelea kuichangia ili kuisaidia
isikwame kwenye maandalizi yake.
Kuendelea kuichangia
-Tuendelee kuichangia Serengeti
Boys hakuna senti itakayopotea
matumizi ya pesa hizo yatakuwa kwa
ajili ya maandalizi ya timu hiyo
isikwame ,tuna matumaini makubwa
timu hiyo itafanya vizuri na
hatutaishia tu Gabon tutaenda na pia
Índia kombe la dunia, ameongeza
Mwakyembe. Serengeti Boys
wanawakilisha Taifa katika Michuano
ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana
wasiozidi Umri wa Miaka 17 nchini
Gabon ambapo wanaendelea kujifua
Kabla ya Kuanza kwa michuano hiyo
Mei 15 mwaka huu.

Chapisha Maoni

 
Top