SHIRIKISHO la Soka la
Kimataifa (FIFA) limethibitisha
mpango wa kuchunguza
uhamisho wa Pauni Milioni
89.3 za kiungo Paul Pogba
kutoka Juventus kwenda
Manchester United msimu
huu.
Bodi ya Sheria ya FIFA
imewasiliana na United
kuomba ufafanuzi kutoka Old
Trafford ikiwemo juu ya
madai kwamba wakala wa
Pogba, Mino Raiola amevuna
kiasi cha Pauni Milioni 41
katika dili hilo.
Inadaiwa mchezo mchafu
umefanyika katika uhamisho
wa wachezaji wote, Pogba na
Zlatran Ibrahimovic aliyetua
United pia msimu huu.
Taarifa za ndani kutoka FIFA
zimesema kwamba kwa
muda sasa United imeombwa
kutoa ufafanzi wa hatua za
mwisho za usajili wa Pogba.
Inafahamika kwamba,
makubaliano ya Raiola na
Juventus kupata asilimia 50
katika usajili wowote
utakaozidi dau la Pauni
Milioni 40 unavunja kanuni
za umiliki wa mmiliki wa mtu
tatu.
Msemaji wa United
ssmesema; "Hatuzungumzii
mikataba, FIFA ilikuwa na
makabrasha tangu uhamisho
ulipokamilishwa Agosti
mwaka jana.'
Makabrasha yote yanapaswa
kupitishwa kwenye mfumo
wa usaili wa FIFA na
hayakuwahi kuonyesha tatizp
lolote hadi sasa.
Chapisha Maoni