Timu ya Tanzania ya kandanda ya wachezaji chipukizi Serengeti Boys Jumanne wiki hii imepata udhamini wa $22,000 kutoka kwa kampuni ya
SportPesa.
Kampuni hiyo ilitangaza udhamini huo wakati ikizindua rasmi huduma ya uchezaji wa kamari kwa kubashiri mechi za kandanda nchini Tanzania.
Mwandishi wa BBC John Nene anasema udhamini huo wa Serengeti Boys utawasaidia sana wakati huu wanashiriki mashindano ya wachezaji chipukizi nchini Gabon.
Waziri wa Mawasiliano, Utamaduni na Michezo nchini Tanzania Harrison Mwakyembe, akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi
huo, amesema wanakaribisha SportPesa nchini Tanzania sio kuendeleza michezo tu lakini
kuanzisha miradi ambayo itawezesha raia wa nchi hiyo kupata ajira.
"Ninawahakikishia ushirikiano wetu, karibuni kwa nchi hii ya michezo,'' amesema Mwakyembe, na
kuongeza: "Huu ndio wakati mwafaka wa kuendeleza michezo humu nchini tukiwa na wenzetu wa SportPesa ambao nina hakika
wataendeleza michezo mingine pia sio kandanda pekee.''
Mkurugenzi wa usimamizi wa kampuni ya SportPesa nchini Tanzania, Abbas Tarimba
amesema haya: "Tunanuia kubadilisha sura ya michezo nchini Tanzania. Naomba wananchi wa
Tanzania muwe watulizu hadi Jumamosi tutakapotangaza rasmi ni timu zipi zitadhaminiwa
na SportPesa.
"Tanzania ina wachezaji wengi wana vipaji (kama Mbwana Samatta), na miezi michache ijayo tuna
mipango ya kuanzisha miradi mikubwa ya kandanda.''
Mkurugenzi kaimu wa mamlaka ya uchezaji kamari nchini Tanzania, James Mbawe, ametangaza rasmi
SportPesa wamepewa leseni ya kamari baada kutimiza masharti yao yote.
Amesema Mbawe: "Uchezaji kamari kupitia michezo umepiga hatua kubwa nchini Tanzania na
kuletea taifa letu mapato zaidi ya dola milioni tisa mwaka wa 2015 na 2016.
"Miaka minne iliyopita wenyeji walikua wanatizama kandanda kujifurahisha lakini sasa watu
wanatizama na kutabiri matokeo ya mpira wa miguu, na hii imewapa vijana ajira na kuendeleza
miradi ya kijamii.''
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni