0
TIMU ya taifa ya vijana chini
ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys inatupa kete
yake ya kwanza katika
michuano ya Mataifa ya
Afrika, itakapomenyana na
mabingwa watetezi, Mali
Uwanja wa l’Amitie Sino
mjini Libreville, Gabon.
Kocha Mkuu wa Serengeti
Boys, Bakari Nyundo Shime
amesema leo mjini
hapa kwamba baada ya
maandalizi mazuri ya muda
mrefu, sasa wako tayari
kuwafurahisha Watanzania.
Lakini Shime amesema
wanakutana na timu nzuri,
ambayo bingwa mtetezi wa
mashindano haya, hivyo
kabisa wanatarajia ushindani
mkali.
“Utakuwa mchezo mgumu,
Mali ndiye bingwa mtetezi wa
haya mashindano na pia
tumewafuatilia kwa kweli ni
timu nzuri sana. Ila tu
niseme sisi tumejipanga
vizuri,”amesema.
Serengeti Boys ilitua Gabon
mapema wiki iliyopita
ikitokea Cameroon ambako
ilikuwa kambi ya wiki moja
na kucheza michezo miwili
ya kujipima nguvu dhidi ya
wenyeji, ikishinda moja 1-0
na kufungwa moja 1-0 pia.
Na ikumbukwe Serengeti
Boys ilikwenda Cameroon
ikitokea mjini Rabat nchini
Morocco ambako iliweka
kambi ya mwezi mmoja
kujiandaa na michauno
inayotarajiwa kuanza Mei 14
hadi 28.
Pamoja na kambi ya
mazoezi, Serengeti Boys
ikiwa mjini Rabat, Morocco
ilicheza mechi mbili za
kirafiki dhidi ya Gabon na
kushinda 2-1 kila mchezo.
Awali Serengeti Boys iliifunga
Burundi mara mbili, Machi 30
mabao 3-0 na Aprili 1 mabao
2-0, mechi zote mbili
zikipigwa Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba, kabla ya
kulazimishwa sare ya 2-2 na
Ghana ‘Black Starlets’ Aprili
3 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Michuano hiyo ilianza rasmi
jana kwa wenyeji, Gabon
kufungwa 5-1 na Guinea,
wakati Ghana nayo iliilipua
Cameroon 4-0.

Chapisha Maoni

 
Top