Usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe amesema
kwamba ameamua kujitoa
kwenye uongozi klabu hiyo
kuepuka kuwa sehemu ya
watu wasio waungwana.
Akizungumza na
Sports Hans
Poppe amesema kwamba
uongozi wa Simba chini ya
Rais wake, Evans Elieza
Aveva umemfanyia mambo
yasiyo ya kiungwana,
mwanachama Mohammed
‘Mo’ Dewji.
Hans Poppe amejiuzulu
Ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Simba na maana
yake amejivua pia na
uongozi wa Kamati ya Usajili
na ya ujenzi wa Bunju
Complex baada ya
kuchukizwa na kutohusishwa
katika mkataba wa udhamini
wa kampuni ya SportPesa.
Zacharia Hans Poppe (kulia)
amesema hataki kuwa
sehemu ya watu wasio
waungwana Simba
“Siyo kushirikishwa mimi tu,
bali Wajumbe wengine wa
Kamati ya Utendaji pia, lakini
kubwa zaidi tuna
makubaliano na Mo (Dewji)
kuwa tukitaka kuingia
mkataba na yeyote Yule,
hakatai lakini tumshirikishe,
sasa tunasaini mkataba kwa
kumzunguka ni kukosa
uungwana na siwezi kuwa
sehemu ya hilo,”amesema.
Poppe amesema kwamba
alijaribu sana kutaka
kukutana na viongozi wa
Simba kujadili nao suala hilo,
lakini walikuwa wanamkwepa
ndiyo maana ameamua
kujiuzulu; “Hatujakaa, kila
nikiwaambia tulijadili
wanaingilia huku wanatokea
kule,”.
Dewji anayetaka kununua
hisa Simba, amesikitishwa na
uongozi wa klabu hiyo kwa
kuingia mkataba wa
udhamini na kampuni ya
SportPesa bila
kumshirikisha.
Na habari ambazo
hazijathibitishwa na upande
wowote, zinasema Mo Dewji,
Mbunge wa zamani wa
Singida Mjini ameuandikia
barua uongozi wa klabu hiyo
chini ya Rais wake, Evans
Aveva kudai alipwe fedha
zake, Sh Bilioni 1.4
alizokuwa anaikopesha
Simba kwa kulipa mishahara
ya wachezaji na benchi la
Ufundi, Sh Milioni 80 kila
mwezi.
Imedaiwa Mo Dewji alikuwa
anatoa fedha hizo kwa
makubaliano zitalipwa wakati
mpango wake wa kununua
hisa za klabu
utakapokamilika. Mo
alikubaliana na uongozi wa
Simba kununua asilimia 51
ya hisa kwa Sh. Bilioni 20
mara baada ya mchakato wa
mabadiliko ya Katiba
utakapokamilika.
Lakini zoezi hilo linaelekea
kuingia doa baada ya Mo
Dewji kuandika katika
ukurasa wake wa Twitter
akilalamikia uongozi wa
klabu kuingia mkataba na
SportPesa bila
kumshirikisha.
Na upande mwingine,
uongozi wa Simba na
umemeguka baada ya Hans
Poppe naye kuandika barua
ya kujiuzulu, naye pia
akilalamikia kutoshirikishwa
katika mkataba wa
SportPesa.
Chapisha Maoni