0
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya
Vijana Chini ya Umri wa Miaka 17
'Serengeti Boys' Bakari Shime
amesema kuwa walishindwa kupata
ushindi dhidi ya Timu ya Mali katika
mchezo wao wa kwanza wa Michuano
ya Kombe La Mataifa ya Afrika
yanayoendelea nchini Gabon kwa
kuwa hawakuwa wamewafahamu
wapinzani wao.
Shime amesema Mali ni timu nzuri na
ambayo ina uzoevu hivyo
anwapongeza wachezaji wa Serengeti
Boys kwa kuonyesha kiwango kizuri.
Hatukuwa tukiwafahamu Mali
-Tatizo kubwa ni kuwa hatukuwa
tukiwafahamu wapinzani wetu na Hii
ilichangia sisi kushindwa kufanya
vizuri katika kipindi cha kwanza,
tuliwasoma na mambo yakabadilika
kipindi cha pili na tuliweza
kuwadhibiti", amesema Shime.
Hata hivyo Shime amewapongeza
wachezaji wake kwa kuonyesha
kiwango kizuri licha ya timu hiyo
kukabiliwa na majeruhi wengi na
kusema wamejifunza mengi kupitia
mchezo wa Mali.
Tumejifunza mengi
-Nawapongeza wachezaji Wangu kwa
kuonyesha mchezo mzuri, Mali ni
Timu nzuri na wana uzoevu,
tumejifunza mengi kupitia mchezo
huo tutayafanyia kazi mapungufu yetu
Kabla ya kukutana na timu ya Angola
katika mchezo ujao tutajitahidi Ili
kupata ushindi licha ya kuwa tuna
majeruhi wengi lakini nawaambia
watanzania wasihofu tumejipanga tuna
wachezaji wakutosha kujaza nafasi
kwa wale watashindwa kucheza",
ameongeza Kocha huyo.
Alama 1
Kufikia sasa kundi hilo la B timu zote
zina alama moja baada ya Timu ya
Guinea kulazimishwa sare ya mabao
2-2 na Angola katika mchezo wa pili
wa kundi hilo.
Michuano hiyo ilianza Jumatatu kwa
Wenyeji Gabon kuchezea kichapo cha
mabao 5-1 dhidi ya Guinea wakati
Ghana wakiwafunga Cameroon kwa
mabao 4-0.

Chapisha Maoni

 
Top