0

Mbao ipo katika hatari ya kushuka daraja, na kocha wa timu hiyo Etienne Ndayiragije amesema
lazima wafe na Yanga Kocha wa timu ya Mbao FC, Etienne
Ndayiragije ameahidi kufa na Yanga kwenye mchezo wao wa mwisho kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu huu.
Ndayiragije  ameiambia Goal , anatambua kuwa Yanga wana hasira nao baada ya kuwafunga na
kuwatoa kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA, lakini wasijidanganye kulipa kisasi
zaidi ya kuwatumia wao kubaki ligi kuu msimu ujao.
“Hatuwezi kukubali kufungwa mechi tatu mfululizo mbaya zaidi mechi ya mwisho tunacheza nyumbani na timu ambayo tunarekodi ya kuifunga tunapocheza nayo nyumbani kwa
kweli wasijidanganye watalipa kisasi bali wajiandae kwa kipigo kingine,” amesema.
Ndayiragije raia wa Burundi, alisema amejipanga kuhakikisha MbaoFC,  inasalia Ligi Kuu, ili kuwasha moto zaidi kwenye msimu ujao ikiwepo
kushiriki michuano ya kimataifa iwapo wataifunga Simba kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la
FA.
Amesema maandalizi yao kuelekea mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga yanaendelea vizuri na nguvu zao zote kwa sasa wamezihamishia hapo kwa sababu ndiyo mchezo pekee waliobakiwa nao msimu huu kabla ya ligi kumalizika.
Mbao,Toto Africans, African Lyon ni miongoni mwa timu zilizopo katika hatari ya kushuka daraja kuifuata JKT Ruvu, endapo hazitapata
ushindi katika mechi zao za mwisho.
Mbao licha ya kutinga fainali ya Kombe la FA, lakini ipo kwenye janga la kushuka daraja endapo
itapoteza mchezo wake wa mwisho ambao itacheza na Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Chapisha Maoni

 
Top