0

Kocha wa Man City amesema matokeo aliyopata msimu huu angepata akiwa Barca au Bayern
angetupiwa virago kwani asingekuwa na kisingizio
Pep Guardiola amedai kuwa klabu zake za zamani Barcelona na Bayern Munich zingemtupia virago kama angepitia kipindi kigumu kama
alichakabiliana nacho msimu huu akiwa na Manchester City.
Mkongwe huyo wa miaka 46 ametwaa mataji 21 katika kipindi alichofanya kazi kama kocha
Hispania na Ujerumani, na ameshindwa kutwaa taji Ligi Kuu Uingereza.
Timu yake ilitolewa pia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora na Monaco.
"Presha niliyokuwa nayo nilipowasili Barcelona, nikiwa sina cha kutetea katika klabu, kama nisingeshinda ndani ya miezi sita, ningetupiwa
virago," talkSPORT kilimnukuu Guardiola akisema.
"Kama Bayern au Bayern Munich, kushinda ni jambo la lazima. Kama hushindi hawakupi nafasi ya pili. Hapa wamenipa nafasi ya pili na nitajaribu kuitendea haki. Katika hali niliyo nayo sasa, kwenye klabu kubwa ni kutimuliwa kazi tu,
ningetupiwa virago. Kwa hakika.
"Katika klabu nilizofanya kazi awali,
Nisingekuwepo, lakini hapa nimepewa nafasi ya pili na nitajidhatiti kuleta matokeo mazuri."
City watazikabili West Bromwich Albion na Watford katika mechi zao mbili za mwisho msimu huu.


Chapisha Maoni

 
Top