0
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema lengo lake ni kushindi dhidi ya Angola katika mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika
kwa Vijana U17 yanayofanyika Gabon.
Tanzania itaingia katika mchezo huo wa Alhamisi ikishika nafasi ya mwisho katika Kundi B baada ya kutoka suluhu na Mali. Angola inaongoza kundi
hilo ikifuatiwa na Niger huku Mali ikishika nafasi ya tatu.
Akizungumza baada ya timu yake kulazimisha suruhu na mabingwa watetezi Mali katika mchezo
wa kwanza, Shime alisema iwapo watashinda mechi ijayo watajiweka vizuri katika kutimiza ndoto
yao ya kucheza nusu fainali.
“Nina furaha tumeanza vizuri japo hatukupata ushindi, Mali walikuwa vizuri lakini tulifanikiwa kuwadhibiti wasipate goli. Imani yangu ni kushinda
mechi ijayo,”alisema Shime.
Baada ya kucheza na Angola, Tanzania itamaliza mechi za hatua ya makundi kwa kucheza na timu ya taifa ya Niger.
Serengeti Boys itaingia katika mchezo huo dhidi ya Angola huku kukiwa na hatihati ya kuwakosa wachezaji wawili walioumia dhidi ya Mali.
Daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija alisema bado wanawapatia matibabu Abdul Seleman na Ally Hussein Msengi walioumia kwenye mchezo dhidi
ya Mali kabla ya kutoa ripoti kwa benchi la ufundi.
“Bado tunawaangalia hali zao, lakini naweza kusema waliumia, Msengi anaendelea vizuri, tutatoa ripoti kwa walimu ambao kama wanaweza
kucheza mchezo ujao au la,”alisema Mngazija.
Nahodha wa timu hiyo, Issa Abdi Makamba atakosa mashindano hayo baada ya kuumia mguu wakati timu hiyo ikiwa katika maandalizi ya
mwisho nchini Gabon.
Vyanzo vingine vya gazeti hili kutoka ndani ya kambi ya Serengeti Boys vinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa Seleman na Mohammed
Abdallah wakakosa mchezo dhidi ya Angola.

Chapisha Maoni

 
Top