0
Mabingwa Watetezi wa Taji la ligi kuu
soka Tanzania Bara Dar Young
Africans, wameukaribia Ubingwa wa 27
baada ya Kuwafunga Toto Africans
kwa Bao 1-0 katika mchezo uliopigwa
Jumanne ya Mei 16 kwenye uwanja
wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa
umuhimu kwa timu zote ulianza kwa
Kasi huku Yanga wakimiliki kipindi
cha kwanza cha mchezo huo, Huku
Toto Africans wakionekana kuingia na
Mbinu Ya kujilinda zaidi.
Katika mchezo huo Yanga walipata
nafasi za wazi lakini wakapoteza, hadi
Timu hizo zinaenda mapumziko
Yanga 0-0 Toto Africans.
Kipindi cha pili walimu wa Timu zote
walifanya mabadiliko ambayo
yalionekana kuongeza hamasa
mchezo huo huku Toto Africans
wakirejea na mfumo mpya ambapo
ushirikiano kati ya washambuliaji wa
Toto Africans Waziri Junior na Jafari
Mohamedi uliikosesha amani beki ya
Yanga.
Kwa upande wa Yanga wachezaji Amis
Tambwe na Obrey Chirwa walipata
nafasi nyingi za wazi ambapo katika
dakika ya 81 Tambwe alifunga bao
nzuri kutokana na kizaazaa cha
mastraika wa Yanga na Mabeki wa
Toto Africans kumchanganya kipa Wa
Toto.
Kileleni
Kufuatia matokeo hayo Yanga
waongeza wigo wa alama 3 Kileleni
kwa kufikisha alama 68 wakati Toto
Africans wakibaki katika nafasi ya 14
wakiwa na alama 29 wakionekana
wazi kuwa hawatoshiriki ligi Kuu
msimu ujao.
Aidha Ligi Kuu Tanzania Bara itafikia
tamati Jumamosi ya Mei 20 Toto
Africans wakiwa ugenini dhidi ya
Mtibwa Sugar nao Yanga watamaliza
Ligi kwa mchezo wa nyumbani dhidi
ya Mbao Fc ambao pia wako katika
hatari ya kushuka daraja.

Chapisha Maoni

 
Top