0
Msafara wa Timu ya Ruvu Shooting
wenye watu 32 Umepata Ajali asubuhi
eneo la Manyoni Mkoani Singida
wakati wakiwa safarini kuelekea Dar
es Salaam wakitokea Mjini Shinyanga
walipocheza mchezo wa Mwisho wa
ligi dhidi ya Stand United.
Ajali hiyo Imetokea baada ya Gari
kupasuka tairi la mbele Upande wa
Kushoto na kuacha Barabara na
kuingia Porini Kabla ya kusimama.
Mlinzi wa Timu hiyo Hamis Suleiman
amesema watu Wote waliokuwapo
kwenye gari hilo wametoka Salama na
kwamba wanamshukuru Mungu Kwani
Kwa namna Ajali ilivyokuwa
hawakuadhani kama kila mtu
angetoka Salama.
Ni Kudra
-Kwa kweli Tunamshukuru Mungu
tumetoka Salama, Kila mtu haamini
kama tungetoka Salama, Yani ni kudra
za Mwenyezi Mungu Tusaidie Ndizi
zilizotuokoa" Alisema.
Timu hiyo ilikuwa ikitokea Shinyanga
ilipocheza na Stand United ambapo
mchezo huo ulimalizika Kwa Ruvu
Shooting kufungwa Kwa Mabao 2-1.

Chapisha Maoni

 
Top