0

Simba ambao ndio washindi wa pili waligoma kupokea medali kwa madai wanaamini wao ndiyo
mabingwa na malalamiko yao yapo FIFA Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taji la ligi ya Vodacom Tanzania Bara, licha ya kupoteza
mchezo wake wa mwisho leo dhidi ya Mbao FC.
Kipigo hicho kumeifanya Yanga kutwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa
lakini inalingana kwa pointi na Simba wote wakiwa na pointi 68 katika michezo 30 waliyocheza.
Yanga iliyoshinda michezo minne mfululizo leo ilikuwa na uhakika mkubwa wa kulipa kisasi cha
kutolewa na Mbao kwenye michuano ya FA, lakini
walijikuta wakiruhusu bao la mapema dakika ya 22 mfungaji akiwa Habibu Hajji.
Yanga walipambana kufa na kupona kutafuta bao la kusawazisha lakini Mbao waliweza kuwadhibiti
vizuri kutokana na kocha wao kujaza viungo wengi kwenye eneo la katikati.
Kipindi cha pili Yanga walihamia kwenye lango la Mbao na kushambulia mfululizo lakini wenyeji wao walibaki kulinda lango lao na kumbakisha mchezaji mmoja pekee mbele.
Ushindi huo umeisaidia Mbao kunusurika na janga la kushuka daraja ikiwa ni miongoni mwa
timu tatu zilizonusurika siku ya mwisho nyingine ni Majimaji na Mbeya City.
Wakati Yanga wanasherekea ubingwa timu za African Lyon na Toto Africans zimeungana na
JKT Ruvu kushuka daraja baada ya kupoteza mechi zao za mwisho zilizochezwa leo.
Kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Mwadui FC, na kufikisha pointi 68 sawa na
Yanga.
Mabao ya Simba leo yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 18, na bao la pili limefungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 26, wakati lile la
Mwadui limefungwa na Poul Nonga.
Simba ambao ndio washindi wa pili waligoma kupokea medali kwa madai wanaamini wao ndiyo
mabingwa kutokana na kupeleka malalamiko yao ya kupokwa pointi tatu FIFA, baada ya Shirikisho
la soka Tanzania TFF, kuwapa Kagera licha ya kumchezasha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu
za njano.
Nayo Kagera Sugar ikiwa ugenini uwanja wa Azam Complex imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Azam 1-0 bao la Kagera likifungwa na Themi Felix.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo ambazo zilikuwa za funga dimba Stand United 2-1 Ruvu Shooting
Tanzania Prisons  0-0  African Lyon
Ndanda    2-0  JKT Ruvu
Majimaji   2-1  Mbeya City
Mtibwa Sugar 3-1  Toto Africans


Chapisha Maoni

 
Top