0
Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka ya
Tanzania 'Taifa Stars', Salum Shabani
Mayanga amewajumuisha
washambuliaji Abdularhaman Musa na
Mbaraka Yusuph katika kikosi
alichokitangaza kwa ajili ya mechi ya
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya
Lesotho.
Kikosi hicho cha wachezaji 24 pia
kimewajuisha Thomas Ulimwengu
ambaye amekuwa na Majeraha ya
Mara kwa Mara pamoja na Nahodha
Mbwana Samatta.
Kikosi kamili.
Kikosi kamili Makipa ni Aishi Manula
kutoka Azam, Benno Kakolanya wa
Yanga na Said Mohammed wa Mtibwa
Sugar, Mabeki ni Shomari Kapombe
Wa Azam, Hassan Kessy wa Yanga,
Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ wa
Simba, Mwinyi Haji wa Yanga, Salim
Mbonde kutoka Mtibwa Sugar, Abdi
Banda wa Simba na Erasto Nyoni
akitokea Azam.
Viungo ni Himid Mao (Azam), Jonas
Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba),
Muzamiru Yassin (Simba), Simon
Msuva (Yanga), Shiza Kichuya
(Simba), Farid Mussa (Tennerife,
Hispania) na Abubakar Salum
( Azam).
Huku Washambuliaji ni Mbwana
Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas
Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden),
Ibrahim Ajibu (Simba), Mbarak Yussuf
(Kagera Sugar) na Abdulrahman
Mussa (Ruvu Shooting),

Chapisha Maoni

 
Top