0
Wachezaji 20 na Viongozi 13 wa
kikosi cha Maafande wa Ruvu
Shooting wapo tayari Mjini Shinyanga
kwa ajili ya mchezo wa ligi Kuu Soka
Tanzania Bara dhidi ya Stand United
'Chama la wana'.
Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau
Bwire amesema wachezaji wameahidi
ushindi katika mchezo huo Licha ya
kuwa wapo katika nafasi Salama.
-Tumezungumza na wachezaji Leo
Jioni baada ya Mazoezi na
wametuahidi ushindi katika mchezo
huo, hatuna la kupoteza Lakini ushindi
Kwetu ni muhimu Sana, Tunataka
kuweka Heshima na lazima Heshima
iwekwe' Masau Alisema.
Kulipiza kisasi.
Aidha Masau amesema kuwa
hawatakuwa na nia ya Kulipiza kisasi
katika mchezo huo Kwani Wanaamini
Mpira wa Miguu si wa Visasi.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika
katika uwanja wa CCM Kambarage
Mjini Shinyanga ikiwa ni kumbukumbu
ya mwaka 2015 ambapo Stand United
waliwashusha daraja Ruvu Shooting
baada ya kuwachapa Bao 1-0.

Chapisha Maoni

 
Top