wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta usiku wa jana
amecheza vizuri kwa dakika
zote 90 timu yake, KRC Genk
ikilazimisha sare ya 1-1
ugenini dhidi ya Lokeren
Uwanja wa Daknam mjini
Lokeren, Ubelgiji kwenye
mchezo wa Kundi B kuwania
tiketi ya kucheza michuano
ya UEFA Europa League
mwakani.
KRC Genk walitangulia kwa
bao la penalti la kiungo
mkongwe wa umri wa miaka
33, Mbelgiji Koen Persoons
aliyejifunga dakika ya nne,
kabla ya mshambuliaji
mwenye umri wa miaka 31,
Mbelgiji pia Tom De Sutter
kuisawazishia Lokeren dakika
ya 57.
Pamoja na sare hiyo, Genk
inaendelea kuongoza Kundi
B katika mchuano wa
kuwania tiketi ya Europa
League mwakani kwa
kufikisha pointi 26 baada ya
kucheza mechi tisa na
Samatta jana ameichezea
Genk mechi ya 58 tangu
ajiunge nayo Januari mwaka
jana kutoka TP Mazembe ya
DRC akiwa amefunga mabao
19.
Kati ya mechi hizo 58,
michezo 18 Samatta alicheza
msimu uliopita na 40 msimu
huu na kati ya hiyo, ni
michezo 36 tu ndiyo alianza,
10 msimu uliopita na 26
msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo
alitokea benchi, nane msimu
uliopita na 13 msimu huu,
wakati 11 hakumaliza baada
ya kutolewa, tano msimu
uliopita na sita msimu huu
na katika mabao hayo 19, 14
amefunga msimu huu na
tano msimu uliopita.
Kikosi cha Lokeren kilikuwa:
Verhulst, Skulason, Single,
De Sutter/Enoh dk65, Terki,
Huppert/Rocketman Stra
dk76, Ticinovic, Rassoul/
Martin dk63, Miric, Knight na
Monsecour.
KRC Genk : Ryan, Nastic,
Wouters, Seigers, Castagne,
Berge, Kumordzi/Heynen
dk61, Sabak/Writers dk76,
Naranjo, Buffalo/Vermijl dk45
na Samatta.

Chapisha Maoni