Barcelona na Real Madrid zote zina fursa sawa kutwaa taji la La Liga na Luis Suarez ameahidi kuendelea kuwatia presha Los Blancos
Nyota wa Barcelona Luis Suarez aapa timu yake itapambana kuendelea kuitia presha Real Madrid
hadi dakika ya mwisho siki ya mwisho La Liga baada ya ushindi dhidi ya Las Palmas.
Vinara hao wa ligi wamejipatia ushindi wa 4-1 Jumapili kupitia hat-trick ya Neymar na moja
akifunga Suarez.
Lakini Real Madrid bado wana mchezo mmoja mkononi na sasa wanahitaji pointi nne tu katika
mechi zao mbili za mwisho ugenini dhidi ya Celta Vigo na Malaga, baada ya kuifunga Sevilla 4-1
kuusogeza ubingwa karibu na mikono yao.
"Tunachopaswa kufanya sasa ni kushinda dhidi ya Eibar jambo litakalowalazimu Madrid kushinda
dhidi ya Celta na Malaga," Suarez aliwaambia waandishi baada ya mechi.
"Itategemeana na kile watakachofanya Jumatano
na Jumapili. Tunatambua kwamba msimu ni mrefu. Tulitaka kuwa na mnyumbuliko mzuri kumaliza vizuri msimu na sasa tuko katika njia
sahihi.
"Tulijua kwamba mechi hii ingekuwa ngumu mbele ya mashabiki wa Las Palmas, lakini tulistahili pointi tatu.
"Tulikuwa na matatizo kidogo kwenye safu ya ulinzi lakini wamefanya kazi nzuri. Tumecheza
vizuri kipindi cha kwanza na hatukufanya makosa mbele ya goli."
Suarez aliulizwa ni kwanini aliamua kumpigia pasi Neymar kufunga goli la kwanza badala ya kupiga mwenyewe wakati nafasi ilikuwa wazi kwake.
"Tupo hapa kuisaidia timu na kushinda ligi," alisema. "Niliona mwenzangu alikuwa kwenye
nafasi nzuri zaidi kuliko mimi na ndio maana nilifanya vile."
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni