Timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Umri
wa miaka 17, Serengeti Boys
imefanikiwa kupata alama Moja dhidi
ya Mali, katika mchezo wa Kwanza wa
Kundi B la michuano ya Afrika kwa
Vijana, mchezo uliofanyika katika
Uwanja wa Stade de l'Amitié Sino-
Gabonaise, Mjini Libreville Nchini
Gabon, baada ya kutoka sare ya 0-0.
Serengeti boys waliuanza mchezo huo
Taratibu kwani katika kipindi chote
cha kwanza walishindwa kutengeneza
nafasi nyingi huku Mali wakiwa bora
zaidi lakini Safu ya Ulinzi ya Serengeti
Boys ilizuia hatari zote zilizoelekea
Upande wao.
Bao limekataliwa.
Ilikuwa ni dakika ya 32 ambapo Mali
walifanikiwa kuzigusa nyavu za mlinda
Mlango wa Serengeti Boys, Ramadhan
Kabwili lakini Mwamuzi Ferdinand
Udoh Aniete kutoka Nigeria akashiria
madhambi kutendeka kabla ya mpira
huo kuzama nyavuni.
Kipindi cha pili benchi la Ufundi la
Serengeti boys lililochini ya Kocha
Mkuu Bakari Shime lilifanya
mabadiliko ya Kiufundi ambapo
waliwaingiza Patrick Mwenda na Abdul
Seleman kuchukua nafasi ya Kiungo
Mkabaji Shaban Ada na Winga wa
kulia Mohamed Abdallah.
Mabadiliko hayo yaliamsha ari kwa
wachezaji wa Serengeti Boys ambao
walianza kucheza kwa kuonana na
kupiga basi za haraka kufanya
mashambulizi ya kushtukiza hata
hivyo walikosa umakini kwani mnamo
dakika ya 65 Mali walifanikiwa
kuisasambua ngome ya Serengeti,
lakini mpira wa kichwa ulipaa nje
kidogo ya lango la Tanzania.
Hadi filimbi ya Mwisho Timu ya Taifa
ya Tanzania Serengeti Boys na Timu
ya Taifa ya Mali ambaye ndiye Bingwa
Mtetezi wa Kombe hilo ziligawana
alama moja baada ya Sare ya 0-0,
ukiwa ni mchezo wa Kwanza wa kundi
B.
Tanzania watashuka Dimbani katika
mchezo wa Pili Mei 18 kucheza na
Timu ya Taifa ya Angola katika
mchezo ambao utafanyika katika
Dimba hilohilo lililopo Libreville nchini
Gabon.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni