sababu ya kuchelewa kupeleka Shauri
la kunyimwa Alama Tatu baada Kagera
Sugar kumchezesha Mohamed Fakhi
akiwa na kadi tatu za njano katika
mahakama ya Michezo 'CAS'.
Simba ambao Walisema watapeleka
suala hili CAS kutokana na Danadana
zinazoendelea Kwani wanafahamu
kuwa kikanuni Kagera Sugar walikuwa
wameenda Kinyume Lakini Kamati ya
Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji
ilizirudisha Alama Tatu kwa Kagera
Sugar wakati tayari Kamati ya Saa 72
ikiwa imekwisha fanya Maamuzi.
Akizungumza na Futaa.co.tz Makamu
Mwenyekiti wa Simba SC Geofrey
Nyange Kaburu, amesema watapeleka
suala hilo Mara tu watakapokamilisha
kukusanya ushahidi pamoja na
vielelezo vyote vinavyohitajika.
Nia
-Nia ya kupeleka kesi yetu CAS sio
kutafuta ubingwa lakini haki yetu
mpira ni wa FIFA, hii pia itasaidia TFF
kufanya kazi kwa weledi kwa Kufuata
Kanuni na sheria za soka, kumekuwa
na mambo mengi yamekuwa
yakijitokeza lakini tukitafuta majibu
Hatuyapati' Kaburu Alisema nia ya
Kupeleka suala Hilo mbele zaidi.
Kaburu amesema kuwa taratibu zote
ziko tayari na kuwa wanasubiri
mamlaka kutoka TFF ili kesi yao ianze
kusikilizwa.
-Taratibu zote zimekamilika
tunasubiri ruling kutoka kwa Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ili
Kuanza kesi yetu' ameongeza
Kaburu.
Umuhimu
Kwa wale ambao wanapinga hatua
hiyo na kusema pesa ambazo
zitatumika kwa kesi hiyo zitumike
katika uendeshaji wa klabu hiyo
Kaburu amesema wanataka kupata
haki na ni muhimu na ndio sababu
wamefikia hatua hiyo.
Klabu ya Simba waliamua kupeleka
kesi yao FIFA baada ya Kamati ya
Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji
kuwapoka pointi tatu ambazo Kamati
ya Masaa 72 ilikuwa imewapoka
Kagera na kuwapatia Simba kwa
madai Kagera Sugar walimchezesha
mchezaji Mohamed Fakhi ambaye
alikuwa na kadi tatu za njano kinyume
na Kanuni za Ligi Kuu Soka Tanzania
Bara.
Chapisha Maoni