(TFF) limevitaka baadhi ya vyombo
vya habari nchini kuacha mara moja
kampeni za upotoshaji zenye lengo la
kuwachafua viongozi wa juu wa
shirikisho hilo.
TFF imeshtushwa na taarifa
inayoendelea kutolewa kwenye gazeti
moja la kila siku ikidai kuwa kuna
ufisadi ndani ya shirikisho wakati
madai hayo ni ya uongo na yenye
lengo la kujenga mtazamo hasi dhidi
ya shirikisho na viongozi wake.
Gazeti hilo la kila siku limetumia
taarifa ya ukaguzi wa fedha
iliyofanywa na wakaguzi kutoka TAC
kujenga picha kuwa ni ushahidi tosha
wa kuwepo kwa ufisadi ndani ya
shirikisho.
Taarifa ya ukaguzi wa fedha ya TAC
haikuwahi kuituhumu TFF kwa ufisadi.
Taarifa ilibaini maeneo ya kiuhasibu
ambayo yalihitaji maelezo ya ziada ya
namna baadhi ya malipo
yalivyofanyika (audit queries), na
ufafanuzi ulitolewa kwa ufasaha na
watendaji wa shirikisho na kupelekwa
mbele ya Mkutano Mkuu wa
Shirikisho.
Misingi ya uandishi.
Hata hivyo gazeti hilo ambalo
limeonekana kuweka kando kabisa
misingi ya uandishi wa habari,
limechapisha taarifa bila hata kutoa
nafasi kwa wanaotuhumiwa kujibu na
kutoa ufafanuzi stahiki.
Rais na katibu mkuu wa shirikisho
wanahudhuria mikutano ya CAF nje ya
nchi wakati gazeti hilo likiendelea
kuporomosha mlolongo wa tuhuma
bila kutoa haki ya kusikilizwa kwa
wanaoandikwa vibaya.
Uchaguzi wa TFF.
TFF inaliangalia suala hili kama
kampeini chafu inayofanywa ili
kushawishi matokeo ya uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika mwezi Agasti
mwaka huu.
Pia taarifa hii potofu inalenga
kulihamisha taifa kutoka kwenye
masuala ya msingi kama kuiunga
mkono Serengeti Boys kwenye
mashindano ya Afrika na kuanza
kujadili masuala yanayohusiana na
siasa za uchaguzi wa TFF.
Hatua za Kisheria.
TFF kwa sasa inatafakari hatua za
kisheria za kuchukua dhidi ya vyombo
vya habari husika na inachukua nafasi
hii kuvisihi vyombo vya habari kuacha
mara moja kujihusisha na kampeni ya
kuchafuana ambayo ni kinyume na
misingi ya maadili ya uandishi wa
habari.
Chapisha Maoni