Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu ambapo mustakabali wa
mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa. Matokeo ya mkutano huo bado hayajawekwa wazi, lakini maamuzi yanabaki baina ya Wenger na Kroenke na yatategemea pia kikao cha bodi
kitakachojadili suala hilo leo hii.
Bado haijajulikana kama Wenger ataongeza mkataba baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa
miaka 21.
Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi
mpaka hivi sasa.
Mipango ya Wenger ilikuwa kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini hali ilibadilika hivi karibuni baada ya kupingwa na baadhi ya mashabiki wa
klabu hiyo.
Kumaliza pia nje ya timu nne bora na kukosa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao imekua changamoto kwake.
Lakini hali kidogo imekua shwari baada ya kuifunga Chelsea 2-1 katika fainali za kombe la FA siku ya Jumamosi na kumfanya Wenger kuwa
kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye kombe hilo huku Arsenal nayo ikiwa na mafanikio zaidi kuchukua kombe hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni