0

Klabu ya Huddersfield Town imepandishwa daraja
kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza baada
ya kulaza Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
Baada ya kutoka sare 0-0 dakika 120, Town walitakiwa kupiga mikwaju kwa mara ya pili na walikuwa na bahati tena baada ya kulaza pia Sheffield Wednesday kwa mikwaju ya penalti hatua ya nusufainali.
Christopher Schindler aliwashindia Town baada ya
mkwaju wa Liam Moore kupaa angani nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka
ya ligi kuu tangu 1972.
Reading, waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu
ya Town waliokuwa nafasi ya tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya
muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.


Chapisha Maoni

 
Top