0

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewataka wachezaji wenzake
kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la
SportPesa ili kuzima tambo Simba.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni
ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa yataanza kutimua vumbi Juni 5 kwa Yanga kuwavaa Tusker ya Kenye kwenye Uwanja wa Taifa.
Cannavaro amesema mashindano hayo yamekuja
katika wakati mgumu kulingana na changamoto
lukuki zinazowakabili.
“Kwa sababu ni mashindano lazima tushindane hivyo wachezaji niwaombe tujitahidi kadri tunavyoweza kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa
mara ya kwanza kuweke historia.” Cannavaro alisema moja ya changamoto kwao kwa
sasa ni wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kuwa katika majukumu ya timu za taifa na wengine kumaliza mikataba yao huku baadhi yao wakiwa
kwenye mfungo wa ramadhani.
Alisema pamoja na changamoto lukuki, lakini
tutahakikisha tunatwaa ubingwa huo kuzima tambo
za Simba baada ya kutwaa Kombe la FA.


Chapisha Maoni

 
Top