0
Nahodha wa Timu ya Simba SC na
kiungo wa Timu ya Taifa Taifa Stars,
Jonas Mkude hatasafiri na kikosi cha
Taifa Stars ambacho kinatarajia
kuondoka nchini siku ya Jumanne ili
kuelekea Misiri kwa ajili ya kuweka
kambi kwa maandalizi ya mchezo wao
wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Africa
dhidi ya Lesotho.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka
nchini (TFF) Alfred Lukas amesema
kuwa Mkude atalazimika kupumzika
baada ya madaktari wa Timu ya Taifa
kumshauri apumzike.
Madaktari
-Mkude alikuwa tayari kujiunga na
kambi ya Stars na madaktari wa
Muhimbili walimkubalia ila madaktari
wa timu ya Taifa wamemshauri
apumzike asisafiri na timu lakini
wamemtaka kocha asimwondoe
kwenye kikosi na atajiunga nacho
baadae”,Alfred Lukas.
Mkude ambaye aliruhusiwa kuondoka
hopitalini Jumatatu mchana baada ya
hali yake kuimarika alikuwa tayari
kujiunga na kikosi hicho baada ya
madaktari wa hospitali ya Muhimbili
kumfanyia vipimo na kusema hana
matatizo ya kiafya na kuwa anaweza
kurejelea hali yake ya kawaida.
Misiri
Taifa Stars ambayo watatumia ndege
ya Ethiopia Airlines wataondoka
Jumanne saa 10 jioni ili kuelekea
Misri ambapo wanatarajia kuweka
kambi ya siku nane.
Kikosi hicho kitajumuisha wachezaji
21 pamoja na viongozi na benchi la
ufundi la timu hiyo huku mchezaji
Farid Musa anayecheza soka la
kulipwa nchini Uispania akitarajiwa
kuungana na timu hiyo huko Misiri.

Chapisha Maoni

 
Top