0

Batshuayi amemaliza msimu na magoli manne katika mechi tatu za mwisho za ligi, ikiwa ni
pamoja na goli lililoipa Chelsea taji
Mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi amesema yupo tayari kuondoka klabuni kwake kwa mkopo msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameshindwa kumpoka namba Diego Costa katika Stamford Bridge katika msimu ambao Chelsea
wametwaa taji la Ligi Kuu Uingereza, mechi pekee aliyoanza ikiwa ile aliyofunga goli la ubingwa.
AS Monaco, West Ham United na Newcastle United iliyopanda daraja zinataka kumsajili
mchezaji huyo kwa uhamisho wa mkopo ili aweze kupata namba kikosi cha kwanza Ubelgiji kuelekea Kombe la Dunia 2018, na Batshuayi
hana shida na popote watakapompeleka Chelsea.
"Kusema kweli, Siwazi sana kuhusu mustakabali wangu," alikiambia chanzo cha Ubelgiji Het Nieuwsblad.
"Najitahidi kwa asilimia 200. Mengine ni maamuzi ya bodi ya klabu. Mimi ni mchezaji na
nitakwenda popote watakaponituma."
Batshuayi amemaliza msimu na magoli manne katika mechi tatu za mwisho za ligi, ikiwa ni
pamoja na goli lililoipa Chelsea taji.


Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top