amejiinamia Uwanja wa
Emirates leo licha ya ushindi
wa 3-1 dhidi ya Everton
katika mchezo wa Ligi Kuu
ya England, kwa sababu
haijamsaidia kupata nafasi ya
kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya baada ya kumaliza
katika nafasi ya tano, nyuma
ya Liverpool, nafasi ya nne,
Manchester City ya tatu,
Tottenham Hotspur ya pili na
Chelsea waliotwaa ubingwa.
Mabao ya Arsenal
yamefungwa na Hector
Bellerin dakika ya
nane, Alexis Sanchez dakika
ya 27 na Aaron Ramsey
dakika ya 90 na ushei, wakati
la Everton limefungwa na
Romelu Lukaku dakika ya 58
kwa penalti. Laurent
Koscielny alitolewa kwa kadi
nyekundu dakika ya 14
baada ya kumchezea
rafu Enner Valencia na
atakosa fainali ya Kombe la
FA dhidi ya Chelsea

Chapisha Maoni