Africans Yusuph Mehbub Manji
amethibitisha kuwa Barua
inayosambaa mitandaoni imeandikwa
na yeye na kwamba ameamua
Kuachia ngazi kuanzia Mei 20, Mwaka
huu.
Manji akihojiwa na Kipindi cha
Michezo cha Sport HQ kinachorushwa
na Radio EFM amesema hiyo ni Barua
sahihi na hamna haja ya kuijadili
Kwani inajieleza vizuri.
-Taarifa hiyo ni Sahihi na hamna haja
ya kuijadili Kwani inajieleza vizuri,
Nimeamua kujiuzulu" Alisema.
Manji ambaye ameingia madarakani
Tangu Julai 2012 amefika Maamuzi
hayo kama yalivyoandikwa kwenye
Barua yake kuwa uamuzi huo ni hiari
na wala usihushwe na Kitu chochote.
Nimeifanyia mambo mazuri Yanga.
Katika taarifa yake Manji amebainisha
kuwa Amefanya mambo Mengi ndani
ya Klabu ya Yanga wakati wa utawala
wake ikiwemo kupata Heshima kubwa
kitaifa na kimataifa.
Aidha katika Hatua hiyo Manji
amesema Ameiacha Klabu chini ya
Uongozi wa Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga ambaye ataendelea
kuiongoza Yanga hadi pale uchaguzi
wa kumpata Mwenyekiti mpya
utakapotangazwa.

Chapisha Maoni