0
Mshambuliaji Emmanuel Okwi
amefurahi kurejea katika klabu yake ya zamani ya Simba na kuwaahidi mashabiki kufanya vizuri ili kuisaidia timu hiyo
kufanikisha malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na Klabu hiyo Okwi amesema anatambua njaa ya ubingwa walio nayo Simba na hivyo atahakikisha anafanikisha timu hiyo kupata matokeo mazuri.
Nashukuru kurejea Simba
-Nashukuru sana viongozi wangu kwa kunikaribisha tena nimekuja hapa tena ili kufanya kazi na hawa viongozi ambao wana njaa sana ya kupata mafanikio katika msimu ujao, nimekuja kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa wa ligi Kuu na kupambana katika mashindano ya kimataifa”, amesema Raia huyo wa Uganda.
Mohamed Dewji
Aidha Okwi ambaye anajiunga na Simba kwa mara ya tatu akitokea SC Villa ya Uganda amemshukuru Mlezi wa timu hiyo bilionea Mohamed Dewji kwa kufanikisha usajili huo ambao umemuwezesha kurejea Msimbazi.
-Nashukuru sana Boss wangu
Mohamed Dewji kwa kufanikisha mimi kuweza kurejea Simba”, ameongeza nyota huyo wa Timu ya Uganda Cranes.

Chapisha Maoni

 
Top