0
Klabu ya Soka ya Majimaji imesema imelazimika kuwatema wachezaji zaidi ya 10 ili kuweza kuanza katika msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania na mashindano mengine.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Maarufu kwa Jina la Wanalizombe, Humphrey Milanzi amesema kwa baraka kutoka kwa Kocha wao Kally Ongala wameamua Kuwaacha wachezaji hao kutokana na Kuonesha Kiwango Duni msimu uliopita pamoja na utovu wa nidhamu.
Amesema baada ya kuponea chupuchupu kushuka daraja wameona waanze kusuka upya kikosi chao ili kuweza kuleta ushindani zaidi msimu ujao pengine kuchukua Taji mojawapo.
Wachezaji waliobaki.
-Kwa Maana Hiyo sasa Majimaji imebakiwa na wachezaji 13 pekee na Tunataka kuongeza wachezaji 11 wapya kutoka timu nyingine na waliobaki tutawachukua kutoka timu ya vijana" Milanzi Alisema.
Milanzi Aliwataja baadhi ya wachezaji walioachwa ni George Mpole , Peter Joseph, Yussuf Mfanyaje, Ibrahim Tende , Agathon Antony, Sagath Mohamed.

Chapisha Maoni

 
Top