0
Mshambuliaji Mario Balotelli amesaini mkataba wa mwaka moja zaidi wa kuendelea kuichezea Nice, imethibisha klabu hiyo ya Ufaransa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia alihamia Ufaransa akitokea Liverpool akiwa mchezaji huru Agosti mwaka jana baada ya kocha wa klabu hiyo ya England, Juergen Klopp kuthibisha kwamba hana mpango naye ndani ya Anfield.
"Mario Balotelli ataendela kucheza OGC Nice msimu 2017/18. Mtaliano huyo jana Jumapili jioni alisaini mkataba," ilisema Nice katika tovuti yake ya (www.ogcnice.com)
Balotelli alijiunga na Liverpool akitokea AC Milan mwaka 2014, lakini alishindwa kuthibisha ubora wake.
Alifunga bao moja katika mechi 16 za Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza na jambo lililofanywa akarudishwa Milan kwa mkopo msimu wa 2015-16, ambalo nako alifunga bao mmoja katika mechi 20, huku akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Balotelli alirejea katika ubora wake alipotua Nice msimu uliopita akifunga mabao 17, katika mechi 28 na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya tatu katika Ligue 1.
Balotelli anaweza kurejea Merseyside hivi karibuni, kwa sababu Nice ni moja ya timu zinazoweza kupangwa kuchezwa na Liverpool katika mechi za mtoano Agosti katika mechi za kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chapisha Maoni

 
Top