0
Pamoja na Atletico Madrid kuendelea kutumikia adhabu ya kutokusajili hadi Januari mwakani bado wanaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan anatarajiwa kuwa atakuwa amepona goti lake wakati huo hivyo atakuwa katika nafasi nzuri ya kujiunga nao.
Atletico wanahisi wanaweza kumkosa mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kwa sababu kurejea kwake hapo kutamnyima nafasi ya kucheza hadi mwakani wakati mwenyewe lengo lake ni kuichezea Hispania katika Kombe la Dunia 2018.
Katika kipindi cha miezi sita, Costa anatakiwa kutafuta timu ya kucheza kwa mkopo, vinginevyo atapoteza nafasi yake katika timu ya taifa.
Kwa mujibu wa Tuttosport, limedai kuwa Ibrahimovic yuko tayari kufanya kazi na Diego Simeone wakati adhabu yao itakapokuwa imekwisha.

Chapisha Maoni

 
Top